TANZANIA PRISONS YATAMBULISHA KOCHA MBADALA WA MINZIRO


KLABU ya Tanzania Prisons imemtambulisha Hamad Hamisi Ally kuwa kocha wake mpya Mkuu, ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kufundisha timu hiyo katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
“Tumefanikiwa kuingia mkataba wa miaka miwili (2) na Kocha Hamad Hamisi Ally. Kocha Hamad anakuja kuwa kocha mkuu wa timu yetu kuanzia hii leo na uongozi unaimani kubwa juu yake,” imesema taarifa ya Tanzania Prisons leo.
Uongozi wa Tanzania Prisons chini ya Mtendaji Mkuu, Ajabu Adam Kifukwe umemtakia kila la kheri kocha Hamad katika majukumu yake yake mapya.
Hamad anachukua nafasi ya Freddy Felix Minziro aliyeondolewa mapema wiki hii kutokana na mwenendo mbaya wa timu katika Ligi Kuu ikiambulia pointi saba katika mechi tisa za awali, hivyo kujikuta nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kwenye mchujo wa kuwania kubaki.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA