YANGA SC YAIFUATA CR BELOUIZDAD UFUNGUZI MAKUNDI LIGI YA MABINGWA
KIKOSI cha Yanga kimeondoka Alfajiri ya leo kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, CR Belouizdad Ijumaa kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Julai 5 1962 Jijini Algiers.
Yanga wanarejea kwenye Uwanja ambao Juni 3, mwaka huu walikaribia kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika wakiwachapa wenyeji, USM Alger 1-0, lakini wakaangushwa na kanuni ya mabao ya ugenini kufuatia kufungwa 2-1 Dar es Salaam Mei 28.
Safarini Yanga inawakosa wachezaji wake 11 waliopo kwenye timu zao mbalimbali za taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia – Afrika, makipa Abdutwalib Mshery, Metacha Mnata, Djigui Diarra (Mali).
Wengine ni walinzi Nickson Kibabage, Dickson Job, Bakari Mwanyeto, Ibrahim Ahmed ‘Bacca’, viungo Mudathir Yahya, Khalid Aucho (Uganda), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso) na mshambuliaji Clement Mzize – ambao wataungana na timu Algeria.
Comments
Post a Comment