SERIKALI YASAINI MKATABA WA BILIONI 19.7 KUKARABATI UWANJA WA UHURU


SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mkataba na Kampuni ya China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ndiye aliyesaini kwa niaba ya Serikali leo Aprili 25, 2024 Jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kufanyika kwa muda wa miezi 12 na ukigharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 19.7.
Katika hatua nyingine, Katibu huyo Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Msigwa aalizindua toleo Maalum la Mafanikio ya Miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA