NI MAN CITY MABINGWA ENGLAND MARA YA NNE MFULULIZO


TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutetea tena ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa West Ham United mabao 3-1 leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na viungo Muingereza mwenye umri wa miaka 23, Philip Walter Foden mawili, dakika ya pili na 18 na Mspaniola Rodrigo Hernández Cascante (27) dakika ya 59, wakati bao pekee la West Ham United limefungwa na kiungo pia, Mghana Mohammed Kudus (23) dakika ya 42.
Kwa ushindi huo Manchester City inayofundishwa na kocha Mspaniola, Pep Guardiola inamaliza na pointi 91, mbili zaidi ya Arsenal iliyomaliza nafasi ya pili na kuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa mara nne mfululizo katika historia ya Ligi Kuu ya England.
Arsenal imemaliza nafasi ya pili baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton Uwanja wa Emirates Jijini London, mabao yake yakifungwa na beki Mjapan Takehiro Tomiyasu dakika ya 43 na kiungo Mjerumani, Kai Havertz dakika ya 89.
Bao pekee la Everton lilifungwa na kiungo Msenegal, Idrissa Gueye dakika ya 40 na inamaliza na pointi zake 40 nafasi ya 15.
Liverpool imemaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers, mabao ya Alexis Mac Allister dakika ya 34 na Jarell Quansah dakika ya 40 Uwanja wa Anfield.
Pamoja na kuchapwa 5-0 na FT
Crystal Palace Uwanja wa Selhurst Park Jijini London, lakini Aston Villa imemaliza na pointi 68 nafasi ya nne na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa upande wao Crystal Palace ambao mabao yao yamefungwa na mshambuliaji Mfaransa, Jean-Philippe Mateta matatu na kiungo Muingereza, Eberechi Oluchi Eze mawili inamaliza na pointi 49 nafasi ya 10.
Tottenham Hotspur imemaliza na pointi 66 nafasi ya tano baada ya kuichapa Sheffield United 3-0, mabao ya kiungo Msweden Dejan Kulusevski mawili na beki Mspaniola,  Pedro Porro Uwanja wa Bramall Lane mjini Sheffield.
Chelsea imemaliza nafasi ya sita na pointi 63 nafasi ya sita baada ya kuichapa AFC Bournemouth 2-1 na kwa pamoja na Spurs wanafuzu Europa League.
Vigogo wengine, Manchester United wamemaliza na pointi 60 nafasi ya nane wakizidiwa tu wastani wa mabao na Newcastle United.
United imemaliza na ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Brighton & Hove Albion mabao ya beki Mreno Diogo Dalot dakika ya 73 na mshambuliaji Mholanzi, Rasmus Højlund dakika ya 88 Uwanja wa The Amex mjini Falmer, East Sussex.
Timu za Luton Town, Burnley na Sheffield United zimeshuka Daraja.
GONGA HAPA KUTAZAMA MATOKEO YOTE MECHI ZA MWISHO LİGİ KUU ENGLAND NA MSIMAMO


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA