TANZANIA BINGWA MASHINDANO YA SHULE ZA AFRIKA KWA WAVULANA
TANZANIA imefanikiwa kutwaa Kombe la Ubingwa wa Soka kwa Shule za Afrika (ASFC) upande wa wavulana baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Guinea jana Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Nayo Afrika Kusini imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo upande wa wanawake kufuatia ushindi wa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1 na Morocco hapo hapo New Amaan Complex.
Fainali ya michuano hiyo ya siku nne iliyofanyika kuanzia Mei 21 hadi 24, ilihudhuriwa na Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe, ambaye mapema siku hiyo alitembelea Ikulu ya Zanzibar kukutana na Rais wa nchi hiyo Dk. Hussein Mwinyi.
Fainali hizo zilitanguliwa na mechi za kuwania nafasi za tatu, Uganda ikiifunga Tanzania 1-0 kwa wasichana na Senegal wakiifunga Benin kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0.
Baada ya mashindano kuhitimisha, Abel Samson wa Tanzania alitangazwa Mchezaji Bora wa ASFC 2024 kwa wavulana, huku Meryem Oubella wa Morocco akiwa MVP upande wa wasichana.
Kipa Bora Wasichana ni Sphumelele Zibula wa Afrika Kusini na Wavulana ni Mujahid Juma wa Tanzania, Mfungaji Bora
Wasichana ni Shadia Nabrye wa Uganda aliyefunga mabao matatu na Wavulana ni Asmara Keita wa Guinea ambao kila mmoja alifunga mabao matatu.
Tuzo ya mchezo wa Kiungwana Wasichana imechukuliwa na Gambia na kwa wavulana ni Afrika Kusini.
Comments
Post a Comment