ZAMALEK MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA


WENYEJI, Zamalek SC wamefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Renaissance Sportive de Berkane (RSB) usiku wa jana Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, nyota mwenye umri wa miaka 26, Ahmed Hamdi Hussein Hafez dakika ya 23 akimalizia kazi nzuri ya kiungo mwenzake, Ahmed Mostafa Mohamed Sayed ‘Zizo’ wote Wamisri.
Zamalek wanakuwa mabingwa kwa faida ya mabao ya bao ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2 kufuatia kufungwa 2-1 wiki iliyopita kwenye mchezo ya kwanza Uwanja wa Manispaa ya Berkane nchini Morocco.
Huu unakuwa msimu wa pili mfululizo, bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika anapatikana kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya msimu uliopita USM Alger ya Algeria kutoa sare ya jumla ya 2-2 na Yanga ya Tanzania.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA