AZAM FC YAACHA WACHEZAJI WANNE ‘KWA MPIGO’ WAMO WAGENI WAWILI
KLABU ya Azam FC imeachana na wachezaji wake wanne ambao ni mabeki Msenegal, Malickou Ndoye, Edward Charles Manyama na viungo, Ayoub Reuben Lyanga na Mnigeria Isah Aliyu Ndala.
Hao wanafanya idadi ya wachezaji walioachwa rasmi kufuatia kumalizika kwa msimu kufika watano baada ya awali kutangaza na beki Mghana, Daniel Amoah.
Tayari Azam FC imesajili wachezaji watano wapya ambao ni mshambuliaji Adam Omary Adam kutoka Mashujaa ya Kigoma, beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien.
Wengine ni Wacolombia, kiungo Ever Meza kutoka Leonnes ya kwao na mshambuliaji Jhonier Blanco kutoka Aguilas Doradas ya kwao pia, Colombia.
Comments
Post a Comment