AZAM FC YASAJILI KIUNGO ALIYECHEZA LIGI ZA MISRI, SERBIA NA CZECH


KLABU ya Azam FC imemtambulisha kiungo mshambuliaji, Nassor Saadun Hamoud (23) kuwa mchezaji wake mpya wa sita kuekelea msimu ujao.
Taarifa ya Azam FC ambayo msimu ujao pamoja na mashindano ya nyumbani, Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe la CRDB Bank pia itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika - imesem Hamoud amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza.
Hamoud alizaliwa Machi 23, mwaka 2001 Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam na kisoka aliibukia timu ya vijana ya Kagera Sugar, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2017.
Mwaka 2018 alikwenda Tersana ya Misri hadi mwaka 2020 akahamia Zarkovo alikocheza hadi kwa nusu msimu akaenda Šumadija Aranđelovac zote za Serbia, kabla ya mwaka  2021 kupelekwa kwa mkopo Vyškov Czech.
Hamoud ambaye mwaka 2021 aliitwa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 'Ngorongoro Heroes' - msimu  uliopita alirejea nchini na kujiunga na Geita Gold ambayo imeshuka daraja na sasa anahamishia maisha yake ya soka Chamazi.
Anakuwa mchezanji mpya wa pili tu mzawa Azam FC baada ya mshambuliaji Adam Omary Adam kutoka Mashujaa ya Kigoma na wa sita jumla pamoja na wa kigeni.
Wachezaji wapya wa kigeni Azam FC ni beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien, Wacolombia, kiungo Ever Meza kutoka Leonnes ya kwao na mshambuliaji Jhonier Blanco kutoka Aguilas Doradas ya kwao pia, Colombia.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA