BOCCO MCHEZAJI WA KWANZA KUPEWA ‘THANK YOU’ SIMBA SC

MSHAMBULIAJI na aliyekuwa Nahodha wa timu kwa mafanikio kwa misimu kadhaa, John Raphael Bocco amekuwa mchezaji wa kwanza kuachwa Simba SC.
Bocco (34) aliyejiunga na Simba SC mwaka 2017 akitokea Azam FC alicheza nusu ya kwanza tu ya msimu uliomalizika, kabla ya kuumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar. 
Alilikuwa sehemu ya wachezaji wa akiba kwenye mechi ya kwanza ya Mapinduzi dhidi ya JKU Januari 1 mwaka huu Simba SC ikishinda 3-1 na akapangwa aanze mechi ya pili, bahati mbaya akaumia katika mazoezi ya kupasha misuli moto Januari 3 dhidi ya Singida Fountain Gate na ndio akamaliza msimu.
Simba ilishinda 2-0 mechi hiyo ya Kundi B na kwenda Robo Fainali na wakafika hadi Fainali wakafungwa 1-0 na Mlandege Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Tangu aumie Bocco amepewa jukumu la kufundisha kikosi cha timu ya vijana cha Simba chini ya umri wa miaka 17.



Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NYOTA WA SIMBA SC ILIYOFIKA NUSU FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA, ABBAS DILUBGA AFARIKI DUNIA