Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM WINGA wa zamani klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, Abbas Dilunga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake, Chanika, nje kidogo ya Jiji. Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Said Dilunga, mchezaji wa Ruvu Shooting ya Pwani, baba yake amefariki dunia ghafla tu nyumbani Chanika. “Ni kweli mzee ametutoka ghafla tu na msiba upo nyumbani kwake, Chanika”amesema Dilunga ambaye jana tu alikuwa kazini akiichezea Ruvu Shooting ikitoa sare ya 1-1 na Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Abbas Dilunga (kushoto) akiwa na mwanawe, Said Dilunga ambaye anachezea Ruvu Shooting ya Pwani Abbas Dilunga, wa tano kutoka kulia katika kikosi cha Simba SC kilichofika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1974 Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Said Dilunga, mchezaji wa Ruvu Shooting ya PwaniAbbas Dilunga ambaye enzi zake alipewa jina Kisungura kwa ujanja na mbio zake uwanjani, atakumbukwa zaidi kwa kuwemo kwenye kikosi tishio cha Si
Comments
Post a Comment