NYOTA WA ANGOLA AINUSURU TABORA UNITED KUSHUKA DARAJA


TIMU ya Tabora United imenusurika kushuka daraja baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa mwisho wa kuwania kubaki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Shujaa wa Tabora United ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Angola, Patrick Lembo Aufumu aliyefunga mabao yote mawili, la kwanza kwa penaltı dakika ya 27 na la pili dakika ya 55 akimalizia mpira wa adhabu.
Kwa matokeo hayo, Tabora United inaitoa Biashara United kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza katikati ya wiki.
Ikumbukwe Biashara United imetoka ligi ya NBC Championship ambako iliitoa Mbeya Kwanza katika mchezo na Tabora United ilitolewa na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NYOTA WA SIMBA SC ILIYOFIKA NUSU FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA, ABBAS DILUBGA AFARIKI DUNIA