SIMBA SC YATANGAZA RASMI KUACHANA NA HENOCK INONGA BAKA ‘VARANE’


KLABU ya Simba imeachana na beki wa Kimataifa was Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Henock Inonga Baka ‘Varane’ baada ya kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi tangu mwaka 2021 alipowasili kutoka DC Motema Pembe ya kwao, Kinshasa. 
Huyo anakuwa mchezaji wa sita kutemwa Simba baada ya beki mwingine wa katı, Kennedy Wilson Juma, viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda.
Tayari Simba SC imemtambulisha mchezaji mmoja tu mpya, beki chipukizi wa katı, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union ya Tanga.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NYOTA WA SIMBA SC ILIYOFIKA NUSU FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA, ABBAS DILUBGA AFARIKI DUNIA