AZİZ Kİ APIGA MBILI, DUBE MOJA YANGA YATWAA KOMBE LA TOYOTA



MABINGWA wa Tanzania wametwaa taji la kwanza la msimu, Kombe la Toyota baada ya kuwafunga wenyeji, Kaizer Chiefs mabao 4-0 jioni ya leo Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein nchini Afrika Kusini.
Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji mpya, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo dakika ya 25, kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki mawili, dakika ya 45’+3 na 63 na mshambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize ambaye sasa anatumika kama winga, dakika ya 57.
Baada ya mchezo huo, Aziz Ki alitangazwa Mchezaji Bora wa Mechi na kupewa mfano wa hundi ya Randi za Afrika Kusini 5000, zaidi ya Sh. Milioni 7.3 za Tanzania huku Yanga wakikabidhiwa Kombe.


Yanga inakamilisha mechi zake za kirafiki katika ziara yake ya wiki mbili Afrika Kusini, nyingine mbili wakifungea 2-1 na Augsburg ya Ujerumani na kushinda 1-0 dhidi ya TS Galaxy mjini Mpumalanga.
Mabingwa hao Tanzania sasa wanatarajiwa kurejea nchini kwa ajili ya tamasha la Kilele ch Wiki ya Mwananchi Agosti 4 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Baada ya hapo watamenyana na Simba SC katika Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii Agosti 8 Uwanja wa Mkapa.
GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 

Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA