CLATOUS CHOTA CHAMA MCHEZAJI WA KWANZA MPYA YANGA SC


KLABU ya Yanga imemtambulisha kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama kuwa mchezaji wake mpya wa kwanza kielekea msimu ujao.
Chama (33), ambaye amekuwa mchezaji muhimu wa timu ya Taifa ya Zambia tangu mwaka 2015 anajiunga na Yanga baada ya kuitumikia Simba SC kws vipindi viwili kuanzia mwaka 2018
Aliwasili Simba SC mwaka 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya kwao, akacheza hadi mwaka 2021 alipouzwa RS Berkane ya Morocco, kabla ya kurejea Msimbazi mwaka 2022 na sasa anahamishia huduma zake Jangwani.
Kisoka Chama aliibukia ZESCO United ya kwao mwaka 2016, kabla ya kuhamia Al Ittihad ya Mısri mwaka 2017 ambako alicheza kwa miezi kadhaa na kurejea Zambia kujiunga na Lusaka Dynamos.




Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NYOTA WA SIMBA SC ILIYOFIKA NUSU FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA, ABBAS DILUBGA AFARIKI DUNIA