DABO WA AZAM NA N'DAW WA YANGA WAPO TANGA WANASOMEA UKOCHA

Kocha Mkuu wa Azam FC,Youssoupha Dabo wa Azam FC katika mafunzo ya Kozi ya ukocha ya CAF A Diploma Jijini Tanga. 

MAKOCHA Wasenegal, Moussa N'Daw wa Yanga na Youssoupha Dabo wa Azam FC ni miongoni washirikiwa Kozi ya ukocha ya CAF A Diploma inayoendelea kwenye Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mnyanjani Jijini Tanga.
Dabo ndiye Mkuu Azam FC, anayesaidiwa na Mfaransa, Bruno Ferry, wakati N'Daw ni kocha Msaidizi Yanga chini ya Muargentina, Miguel Angel Gamondo na wote wawili hawajasafiri na timu zao kwenye kambi za kujiandaa na msimu kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo hayo.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Moussa N'Dawkatika mafunzo ya Kozi ya ukocha ya CAF A Diploma Jijini Tanga.   

Ikumbukwe Azam FC imeweka kambi nchini Morocco, wakati Yanga wapo Afrika Kusini na timu zote zitaanza na michuano ya timu, Ngao ya Jamii mapema mwezi ujao.
Azam FC itaanza michuano ya Ngao ya Jamii kwa kumenyana na Coastal Union Agosti 8 kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kabla ya Yanga watamenyana na watani wao, Simba SC Saa 1:00 siku hiyo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA