SABA KUIWAKILISHA TANZANIA OLIMPIKI YA PARIS 2024
KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC) imetaja wanamichezo saba watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris inayotarajiwa kuanza Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu.
Hao ni pamoja na Wanariadha wanne Alphonce Felix Simbu na Gabriel Geay, wanaume na Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri wanawake, wote mbio ndefu, Marathon.
Wengine ni Waogeleaji, Sophia Anisa Latiff 50m freestyle (wanawake) na Collins Phillip Saliboko 100m freestyle (wanaume) na Mcheza Judo, Judo Andrew Thomas Mlugu.
Msafara huo uambao utaagwa Ijumaa kabla ya kuondoka Jumapili Alfajiri, utahussha makocha watatu, Daktari mmoja, Maafisa Wawili wa TOC, Mwana Habari mmoja na Mkuu wa Msafara.
Kamati ya Olimpiki Tanzania imetoa shukrani za dhati kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa michango yao kwa timu hiyo.
Comments
Post a Comment