SIMBA SC YASAJILI ALIYEKUWA ANACHEZA LİGİ YA AFRİKA KUSINI


KLABU ya Simba imemtambulisha beki wa kati mzawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini kuwa mchezaji wake mpya wa tano kuelekea msimu ujao.
Hamza ni mchezaji aliyeibukia Mbeya City mwaka 2020, kabla ya kuhamia KMC mwaka 2021 na Namungo FC 2022 ambayo ilimuuza SuperSport mwaka jana.
Wachezaji wengine waliosajiliwa Simba ni beki mzawa, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union, winga Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya Zambia na washambuliaji Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'Adjamé ya kwao.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NYOTA WA SIMBA SC ILIYOFIKA NUSU FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA, ABBAS DILUBGA AFARIKI DUNIA