SIMBA SC YASAJILI MSHAMBULIAJI MGANDA WA ASANTE KOTOKO


KLABU ya Simba imemtambulisha mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana, ambaye aliibukia Vipers SC kabla ya kupelekwa kwa mkopo Maroons FC, zote za kwao, Uganda.
Steven Mukwala anakuwa mchezaji mpya wa tatu Simba SC baada ya beki mzawa, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union ya Tanga na winga Mzambia, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos ya kwao.
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuingia kambini wiki hii nchini Misri kujiandaa na msimu mpya, ambao utafunguliwa kwa Tamasha la Simba Day Agosti 3 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NYOTA WA SIMBA SC ILIYOFIKA NUSU FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA, ABBAS DILUBGA AFARIKI DUNIA