TANZANIA YAPOTEZA MWANAMICHEZO WA PILI PARIS OLIMPIKI 2024
KARATA ya pili ya Tanzania katika mashindano ya Olimpiki ya Paris 2024 imeingia maji leo wakati muogeleaji Collins Phillip Saliboko, alipomaliza katika nafasi ya saba alipojitosa katika bwawa la Paris les Defence Arena na kupambana na ushindani mkali sana katika michuano ya mita 100 (Freestyle) kwa wanaume.
Saliboko ametumia sekunde 53:38 kumaliza mchuolano huo, wakati mshindi wa kwanza Ovesh Purahoo kutoka Mauritius ametumia sekunde 52:22, ikiwa ni tofauti ya sekunde 1:16 tu.
Mhe Waziri ambaye ameshuhudia mwenyewa mchuano huo, amempongeza Saliboko mwenye umri wa miaka 22 kwa juhudi zake ambazo zimemuwezesha kuvunja rekodi yake mwenyewe ya sekunde 52: 54 aliyoiweja kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola mwaka 2022.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Dam as Ndumbaro amemtaka Saliboko, aendeleze juhudi za kufanya mazoezi ili aendelee kuwakilisha nchi katika mashindano makubwa yajayo.
Amemwambia Saliboki anayesoma University of Indianapolis, Marekani kwanba kwa umri alionao bado ana nafasi kubwa ya kufanya vyema siku za usoni.
Waziri pia amemtaka muogoleaji huyo ahakikishe pia kwamba anazalisha kina Saliboko wengine kwa kutumia muda wake wa likizo kuwasaidia waogeleaji chipukizi wafikie viwango vya juu kama yeye.
Karata ya tatu ya Tanzania itatupwa Jumamosi Agosti 3, 2024 na muogeleaji Sophia Anisa Latiff ambaye atashindana katika mita 50 (Freestyle) kwa wanawake mnamo saa 6:00 mchana kwa saa za Tanzania.
Waziri Dkt. Ndumbaro, amemtaka Sophia Anisa Latiff mwenye umri wa miaka 17 ajitahidi kupeperusha bendera ya Tanzania juu zaidi wakati wa kutupa karata ya tatu Agosti 3, 2024 atakapoingia bwawani katika michuano ya mita 50 freestyle kwa wanawake.
Comments
Post a Comment