ABUBAKAR BAKHRESA AKUTANA NA WACHEZAJI AZAM KUWATIA HAMASA WAING'OE APR


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC na Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Bakhresa Group (SSB), Abubakar Said Salim Bakhresa mapema leo ametembelea kambi ya timu Jijini Kigali, Rwanda na kuzungumza na wachezaji kuelekea mchezo muhimu dhidi ya wenyeji, APR.
Azam FC inatarajiwa kushuka Uwanja wa Amahoro Jijini Kigali kuanzia Saa 1:00 usiku kumenyana na timu ya Jeshi la Watu wa Rwanda, APR katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na viongozi wengine wa juu timu, akiwemo Mwenyekiti Nassor Idrisa 'Father', Abubakar amewataka wachezaji kujituma kuhakikisha wanaitoa APR na kufuzu hatua ya 32 Bora.
Nao wachezaji wamemuahidi Abubakar watajtuma kuhakikisha wanapata matokeo mazuri dhidi ya wenyeji na kufuzu hatua inayofuata.
Ikumbukwe mchezo wa kwanza Azam FC iliibuka na ushindi wa 1-0 bao pekee la mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Alfonso Blanco Yus dakika ya 56 kwa penalti kufuatia kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari Jumapili. 
Mshindi wa jumla kati ya Azam ma APR atakutana na mshindi wa jumla kati ya JKU na Pyramids ya Mısri kuwania kuingia hatua ya makundi, 16 Bora.
Pyramids iliichapa JKU 6-0 juzi Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo na marudiano yao ni leo pia hapo hapo Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA