ASHA MWALALA APIGA HAT-TRICK SIMBA QUEENS YASHINDA 5-0


TIMU ya Simba Queens imeanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya FAD ya Djibouti katika mchezo wa Kundi B leo Uwanja wa Abebe Bikila mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Jentrix Shikangwa dakika ya 24, Elizabeth Wambui dakika ya 30 na Asha Rashid ‘Mwalala’ matatu dakika ya 75, 80 na 89.
Simba Queens itashuka tena dimbani Jumatano Saa 8:00 mchana kumenyana na Kawempe Muslim, kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kucheza na PVP Buyenzi ya Burundi Ijumaa Saa 11:00 jioni hapo hapo Abebe Bikila.
GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA