AZAM FC YAIFUATA APR USIKU HUU SHUGHULI NI JUMAMOSI AMAHORO
KIKOSI cha Azam FC kinatarajiwa kuondoka Saa 9 usiku wa leo kwenda Kigali, nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, APR Jumamosi Uwanja wa Amahoro Jijini Kigali.
Afisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria 'Zaka Zakazi' amesema timu inaondoka na wachezaji 22, huku wengine wakikosekana kwenye safari hiyo kipa Ali Ahamada, viungo Yahya Zayd, Sospter Bajana, Abdul Khamis Suleiman 'Sopu' na washambuliaji, Msenegal Alassane Diao na Mcolombia, Franklin Navarro kwa sababu ni majeruhi.
Ikumbukwe mchezo wa kwanza Azam FC iliibuka na ushindi wa 1-0 bao pekee la mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Alfonso Blanco Yus dakika ya 56 kwa penalti kufuatia kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari Jumapili.
Mshindi wa jumla kati ya Azam ma APR atakutana na mshindi wa jumla kati ya JKU na Pyramids ya Mısri kuwania kuingia hatua ya makundi, 16 Bora.
Pyramids iliichapa JKU 6-0 juzi Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo na marudiano yao ni Jumamosi pia hapo hapo Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30.
Comments
Post a Comment