AZAM FC YAITANDIKA COASTAL 5-2 NA KUTINGA FAINALI NGAO YA JAMII


TIMU ya Azam FC imefanikiwa kuingia Fainali ya michuano ya Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Coastal Union jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Mabao ya Azam yamefungwa na winga Mgambia Gibril Sillah dakika ya 13, kiungo Feisal Salum dakika ya 40, washambuliaji Mcolombia Jhonier Blanco dakika ya 45'+1, Adam Omary dakika ya 87 na kiungo Mcolombia, Ever William Meza Mercado dakika ya 90'+2.
Kwa upande wao, Coastal Union mabao yao yamefungwa na kiungo Charles Semfuko dakika ya 27 na  Abdallah Hassan dakika ya 85.
Sasa Azam FC itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya Pili baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga ambazo zipo dimbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam zinapapatuana kusaka tiketi ya Fainali – itakayochezwa Jumapili ikitanguliwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA