CHAMA NA MUSONDA WAFUNGA YANGA YASHINDA 4-1 MECHI YA KIRAFIKI KIGAMBONI


KATIKA kujiandaa na mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’O ya Burundi Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam – Yanga jana ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Green Warriors Uwanja w Avic Town, Kigamboni na kuibuka na ushindi wa 4-1.
Mabao ya Yanga jana yalifungwa na Wazambia, Clatous Chama, Kennedy Musonda, Mkongo Jean Baleke na Mkenya, Duke Abya – na leo kikosi kinarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa Jumamoasi, ambao mechi zote mbili dhidi ya Vital’O zitachezwa Dar es Salaam, wa kwanza Yanga akiwa mgeni Chamazi na marudiano atakuwa mwenyeji Jumamosi ya Agosti 24 Uwanja wa Benjamn Mkapa, Dar es Salaam.
Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati SC Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia (CBE) katika Raundi ya kwanza kuwania kuingia hatua ya makundi, 16 Bora.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA