COASTAL UNION YACHAPWA 3-0 ANGOLA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA


TIMU ya Coastal Union imejiweka njia panda katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-0 na wenyeji, Bravos do Maquis jioni ya leo katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Uwanja wa Taifa wa Tundavala mjini Lubango nchini Angola .
Timu hizo zitarudiana Agosti 25 Uwanja wa Azam Complex na mshindi wa jumla atakutana na St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Simba SC wataanzia Raundi ya Kwanza kwa kumenyana na mshindi kati ya Uhamiaji ya Zanzibar na Al Ahli Tripoli ya Libya.



Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA