COASTAL UNION YAUMALIZA MWENDO KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA MAPEMA TU


TIMU ya Coastal Union imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya kufungana na Bravos do Maquis ya Angola leo katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Wagosi wa Kaya au Wana Mangush kwa majina ya utani wanatupwa nje kufuatia kuchapwa  3-0 na Bravos do Maquis katika mchezo wa kwanza Jumamosi ya wiki iliyopita Uwanja wa Taifa wa Tundavala mjini Lubango nchini Angola.
Bravos do Maquis sasa itakutana na St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Hatua ya 32 Bora kuwania kuingia Hatua ya 16 Bora, inayochezwa kwa mtindo wa makundi.
Wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Simba SC wataanzia Raundi ya Kwanza kwa kumenyana na Al Ahli Tripoli ya Libya iliyoitoa Uhamiaji ya Zanzibar.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA