DICKSON JOB AREJESHWA TAIFA STARS MECHI ZA KUFUZU AFCON




BEKİ wa Yanga, Dickson Nickson Job amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa, Taifa Stars kwa ajili ya Michezo miwili ya Kundi H Kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Ethiopia na Guinea mapema mwezi ujao.
Job aliwekwa kando Taifa Stars baada ya kukaidi agizo la Kocha Hemed Suleiman Morocco kucheza beki ya pembeni, lakini baada ya kuomba radhi sasa amerejeshwa.
Taifa Stars itakuwa mwenyeji wa Ethiopia Septemba 6, kabla ya kusafiri kuwafuata Guinea ambao watachezea nchini Ivory Coast.
Timu nyingine katika Kundi hilo kuwania tiketi ya AFCON ya 2025 itakayofanyika nchini Morocco ni DRC na ambayo itacheza na Taifa Stars Okoba 14 Jjjini Dar es Salaam.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA