DUBE, CHAMA NA AZIZ KI WAFUNGA YANGA YAWACHAPA VITAL'O 4-0 CHAMAZI


MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wametanguliza mguu mmoja hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Vital'O ya Burundi katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya sita, kiungo Clatous Chotta Chama dakika ya 68, msambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize dakika ya 74 na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki kwa penalti dakika ya 90'+1.
Timu hizo zitarudiana Jumamosi ya Agosti 24 Uwanja wa Benjamn Mkapa, Dar es Salaam – na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati Sports Club Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA