FOUNTAIN GATE YAICHAPA NAMUNGO FC 2-0 PALE PALE RUANGWA


TIMU ya Fountain Gate imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Edgar William dakika ya 30 na Suleiman Mwalimu dakika ya 45’+3 huo ukiwa ushindi wa kwanza katika mechi mbili za mwanzo za simu, zote wakicheza ugenini wakitoka kuchapwa 4-0 na Simba Jijini Dar es Salaam Jumapili.
Kwa Namungo FC leo wamepoteza mechi ya pili mfululizo nyumbani baada ya kuchapwa 2-1 na Tabora United katika mchezo wa kwanza. 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA