KMC YARIDHIA UHAMISHO WA AWESU KWENDA SIMBA SC


KLABU ya KMC imeridhia kiungo Awesu Ally Awesu ajiunge na Simba SC baada ya maridhiano kufuatia mazungumzo ya pande zote mbili.
Simba ilimsajili Awesu, lakini KMC ikaweka pingamizi ikidai bado ina mkataba na kiungo huyo.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ikaelekeza Simba iwasiliane na KMC kwa ajili ya kufanya uhamisho wa mchezaji huyo.
Jioni hii KMC imetoa taarifa ya kuridhia uhamisho wa Awesu baada ya kufikia maridhiano na Simba.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA