MECHI YA WATANI LEO; TUTAINGIA NA MBINU TOFAUTI, ASEMA KOCHA WA SIMBA SC


KOCHA Mkuu wa Simba SC, Fadluraghman 'Fadlu' Davids amesema kwamba ataingia na mbinu tofauti kuhakikisha anapata matokeo mazuri dhidi ya watani, Yanga leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, Davids amesema analazimika kufanya hivyo kutokana na uzoefu wake wa mechi za wapinzanina yeye timu yake ni mpya.
"Tunaichukulia hii mechi kama nyingine, tunahitaji kushinda ili kuanza vizuri msimu kwa kulitetea Kombe hili. Nina uzoefu wa michezo hii mikubwa ya wapinzani, ukiangalia timu yetu ni mpya, tutakuja na mbinu tofauti kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,"amesema raia huyo wa Afrika Kusini. 
Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo, Mohamed Hussein 'Tshabalala' amesema kwamba utakuwa mchezo wenye ushindani kwa sababu wanakwenda kukutana na timu yenye wachezaji wazuri, ila malengo yao ni kupata ushindi.
"Kulingana na maandalizi tuliyoyafanya, timu yetu imeimarika zaidi, ila tunaamini tunakwenda kukutana na timu yenye wachezaji wazuri. Utakuwa mchezo wenye ushindani, ila malengo yetu ni kupata ushindi,"amesema.
Simba watamenyana na Yanga  katika Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii leo kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Mkapa na mshindi atakutana na mshindi kati ya Azam FC na Coastal Union zinazomenyana pia leo Saa 10:00 jioni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA