SIMBA NA YANGA NYINGINE JUMAMOSI YA OKTOBA 19 LİGİ KUU


LIGI Kuu ya NBC Tanzania Bara inatarajiwa kuanza rasmi Agosti 16, Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ukipewa heshima ya ufunguzi kwa mchezo baina ya wenyeji, Pamba Jiji FC dhidi ya Tanzania Prisons kuanzia Saa 10:00 jioni.
Vigogo, Simba watashuka dimbani Agosti 18 kumenyana na Tabora United kuanzia Saa 10:15 jioni Uwanja wa Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Dar es Salaam.
Azam FC watacheza mechi yao ya kwanza Agosti 28 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mabingwa watetezi, Yanga wao wataanzia Bukoba Agosti 29 kumenyana na wenyeji, Kagera Sugar kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Kaitaba.
Watani wa jadi watakutana katika mechi ya mzunguko wa kwanza Jumamosi ya Oktoba 19, Simba akiwa mwenyeji na marudiano yatafuatia Jumamosi pia ya Machi 1, Mwaka 2025.
GONGA HAPA KUTAZAMA RATIBA KAMILI YA LİGİ KUU 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA