SIMBA QUEENS YATOA SARE, KUMENYANA NA POLISI YA KENYA NUSU FAINALI CECAFA


TIMU ya Simba Queens imekamilisha mechi zake za Kundi B Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa sare ya kufungana mabao 2-2 na PVP Buyenzi ya Burundi leo Uwanja wa Abebe Bikila mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Mabao ya Simba Queens leo yamefungwa na nyota wake wa Kimataifa wa Kenya, kiungo Vivian Corazone Aquino Odhiambo Vivien na mshambuliaji Jentrix Shikangwa Milimu na kwa matokeo hayo wanamaliza na pointi saba na kuongoza Kundi B mbele ya Kawempe Muslim ya Uganda.
Kawempe imemaliza na pointi sita baada ya ushindi wa 10-0 dhidi ya FAD ya Djibouti leo pia Uwanja wa Abebe Bikila, mabao yake yakifungwa na Hadijjah Nandago matano, Shadia Nabirye mawili, Rebecca Nakato, Halimah Kampi na Mary Kabucurezi moja kila mmoja.
Sasa katika Nusu Fainali, Simba Queens watamenyana na washindi wa pili wa Kundi A, Polisi ya Kenya, wakati Kawempe Muslim watacheza na vinara wa Kundi A, wenyeji CBE FC Jumatatu.



Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA