SIMBA QUEENS YAWAPIGA WAGANDA 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI CECAFA


TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya Wanawake Afrika Mashariki na Kati baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kampe Muslim ya Uganda mchana wa leo Uwanja wa Abebe Bikila mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. 
Mabao yote ya Simba Queens leo yamefungwa na nyota wake wa Kimataifa wa Kenya, mshambuliaji Jentrix Shikangwa Milimu dakika ya 54 na viungo Vivian Corazone Aquino Odhiambo dakika ya 69 na Elizabeth Wambui dakika ya 75.
Kwa ushindi huo, Simba Queens inayofundishwa na wanasoka wa zamani wa kimtaifa wa kiume, Juma Mgunda na Mussa Mgosi inafikisha pointi sita na kuendelea kuongoza Kundi B kufuatia ushindi wa 5-0 dhidi ya FAD ya Djibouti kwenye mchezo wa kwanza juzi.
Simba Queens, mabingwa wa micbhuano hiyo mwaka 2022 watakamilisha mechi zao za Kundi B kwa kumenyana na PVP Buyenzi ya Burundi hapo hapo Abebe Bikila.
Kawemepe Muslim walioshinda 2-0 dhidi ya PVP Buyenzi katika mchezo wa kwanza wao watamaliza na FAD keshokutwa.
Katika Kundi A wenyeji, CBE wanaongoza kwa pointi zao sita, wakifuatiwa na Polisi ya Kenya pointi nne, Yei Joint Stars ya Sudan Kusini pointi moja, wakati Rayon Sport ya Rwanda ambayo imepoteza mechi zote mbili za awali inashika mkia.
Mechi za mwisho za Kundi A zinachezwa kesho Saa 10:00 jioni zote, Yei Joint Stars dhidi ya Rayon Sport na Uwanja wa Abebe Bikila CBE dhidi ya Polisi Uwanja wa Addis Ababa.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA