SIMBA SC YAIRARUA FOUNTAIN GATE 4-0 LEO KINONDONI


TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo mzawa, Edwin Charles Balua dakika ya 13, mshambuliaji Mganda, Steven Dese Mukwala dakika ya 44, kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 58 na mshambuliaji mzawa, Valentino Mashaka Kusengama dakika ya 81.
Ushindi huo wa pili katika mchezo wa pili tu wa msimu unaifanya Simba ifikishe pointi sita na kupanda kileleni ikiizidi wastani wa mabao Singida Black Stars, wakati kwa Fountain Gate leo ilikuwa mechi yao ya kwanza.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA