TANZANIA YAHITIMISHA ‘SALAMA’ USHIRIKI USHIRIKI WAKE OLIMPIKI YA PARIS


TANZANIA imehitimisha ushiriki wake kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu bila kushinda Medali yoyote baada ya Wanariadha wake, Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri kufanya vibaya kwenye Marathoni ya Wanawake katika kilele cha Michezo hiyo iliyoanza Julai 26.
Magdalena Crispin Shauri amemaliza nafasi ya 40 Kati ya wakimbiaji 80 waliomaliza, akitumia muda wa Saa 2 dakika 31 na sekunde 58, wakati Jackline Juma Sakilu ni kati ya wanariadha 11 ambao hawakumaliza mbio hizo.
Mholanzi mwenye asili ya Ethiopia, Sifan Hassan ameshinda Medali ya Dhahabu kwenye Marathoni hiyo akiweka rekodi kwa kutumia muda wa Saa 2 dakika 22 na sekunde 55, akifuatiwa na Tigst Assefa wa Ethiopia na Hellen Obiri wa Kenya katika nafasi ya tatu leo Jijini Paris.
Ikumbukwe jana wakimbiaji wengine wawili wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu na Gabriel Gerald Geay walikimbia Marathoni ya wanaume, ambayo Tamirat Tola wa Ethiopia alishinda Medali ya Dhahabu.
Angalau Simbu alimaliza nafasi ya 17 akitumia muda wa 2:10:03, lakini Geay alikuwa nje ya kinyang'anyiro kabisa akimaliza nafasi ya 74 kati ya wakimbiaji 81.
Wanamichezo wengine watatu wa Tanzania, waogeleaji Collins Phillip Saliboko na Sophia Anisa Latiff pamoja na Mcheza Judo, Andrew Thomas Mlugu wote walitolewa mapema.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA