ABUBAKAR, YUSUF BAKHRESA NA FATHER WAWAKABIDHI TIMU MAKOCHA WAPYA


BODI ya Wakurugenzi ya Azam FC ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Abubakar Said Bakhresa leo imetambulisha benchi jipya la Ufundi  kwa wachezaji na wafanyakazi wa timu.
Benchi hilo linaundwa na  Kocha Mkuu, Rachid Taoussi, Kocha msaidizi, Badr Driss, Kocha wa utimamu wa mwili, Ouajou Driss na Kocha wa makipa, Rachid El Mekkaoui wote raia wa Morocco.
Katika kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya klabu, Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam, Abubakar aliambatana na mdogo wake, Yusuf Bakhresa ambaye ndiye Mkurugenzi Mkuu wa klabu na Mwenyekiti wa klabu, Nassor Idrissa 'Father'.
GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA