AHOUA MCHEZAJI BORA, FADLU KOCHA BORA LIGI KUU MWEZI AGOSTI


KIUNGO wa Simba SC, Muivory Coast Jean Charles Ahoua (22) ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Agosti, huku kocha wake, Fadluraghman 'Fadlu' Davids akishinda Tuzo ya Kocha Bora.
Kwa pamoja, wawili hao, Fadlu na Ahoua wameisaidia Simba kukusanya pointi sita katika mechi za mwanzo za msimu, wakichapa Tabora United 3-0 na Fountain Gate 4-0 Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Dar es Salaam.
Kwa mwezi huo wa kwanza wa msimu, Tuzo ya Ashraf Omar akibeba Tuzo ya Meneja Bora wa Uwanja kwa kazi yake nzuri Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, uliopo Mbweni Jijini Dar es Salaam.
   


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA