AZAM FC YAAMBULIA SULUHU KWA PAMBA JIJI AZAM COMPLEX


WENYEJI, Azam FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Ni sare ya tasa ya pili mfululizo katika mechi mbili za mwanzo za msimu kufuatia sare ya 0-0 pia na JKT Tanzania katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Na kwa Pamba pia ni mfululizo wa sare tatu za mabao katika mechi tatu za mwanzo za msimu pamoja na zile mbili za nyumbani, Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji FC.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA