FOUNTAIN GATE NA DODOMA JIJI ZATOSHANA NGUVU, SARE 2-2 MANYARA


TIMU za Fountain Gate na Dodoma Jiji zimegawana pointi kwa sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Manyara.
Ilikuwa mechi tamu ya funga nikufunge baina ya timu zinazotumia Uwanja wa Tanzanite Kwaraa kama wa nyumbani - mara zote Dodoma Jiji ya kocha Mecky Mexime ikitangulia na Fountain Gate ya kocha Mohamed Muya ikisawazisha.
Mabao ya Dodoma Jiji yalifungwa na washambuliaji na Hassan Mwaterema dakika ya 27 na Paul Peter dakika ya 51, wakati ya Fountain Gate waliokuwa wenyeji leo yamefungwa na Suleiman Mwalimu ‘Gomez’ dakika ya 50 na Dickson Ambundo dakika ya 85.
Baada ya mchezo, Suleiman Mwalimu ‘Gomez’ anayecheza kwa mkopo Fountain Gate kutoka Singida Black Stars aliyeuliwa Mchezaji Bora wa Mechi. 
Matokeo hayo yanaifanya Fountain Gate ifikishe pointi saba na Dodoma Jiji pointi tano baada ya wote kucheza mechi nne.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA