KARIA AKUTANA NA VIONGOZI WAKUU SIMBA NA YANGA KUYAJENGA
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na Makamu wake wa Kwanza wa Rais, Athumani Nyamlani leo wamekutana na Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu na Rais wa Yanga SC, Hersi Said kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo ushiriki wao wa michuano ya Afrika.
Yanga watamenyana na timu ya Benki ya Biashara Ethiopia, CBE SA (Commercial Bank of Ethiopia Sports Association) Jumamosi kuanzia Saa 2:30 katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Yanga ilitanguliza mguu mmoja Hatua ya 16 Bora inayochezwa kwa mtindo wa makundi baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya CBE Jumamosi kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa, siku hiyo bao la Wananchi likifungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 45’+1.
Kwa upande wao Simba SC watamenyana na Al Ahly Tirpoli Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni katika mchezo wao wa marudiano Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Simba inahitaji hata ushindi wa 1-0 ili kusonga mbele, Hatua ya 16 Bora inayochezwa kwa mtindo wa makundi na mambo yatakuwa magumu kama itakuwa sare ya mabao kufuatia mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare ya mabao Jumapili iliyopita Uwanja wa Juni 11 Jijini Tripoli nchini Libya.
Comments
Post a Comment