KIUNGO WA ZAMANI WA YANGA ABDUL MANENO 'DENIS LAW' AFARIKI DUNIA

Abdul Maneno Kibavu, wa kwanza kulia waliosimama katika kikosi cha Yanga mwaka 1998
KIUNGO wa zamani wa klabu ya Yanga, Abdul Maneno Kibavu 'Denis Law' (54) amefariki dunia jana majira ya Saa 5 usiku katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu ya moyo.
Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Maabad Maneno Kibavu, mchezaji huyo amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya Moyo tangu Aprili mwaka huu na matbabu yake yalianza katika Hospitali ya Amana, kabla ya kuhamishiwa Muhimbili, wadi ya Jakaya. 
Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Gombero, Magomeni Mwembechai Jijini Dar es Salaam na mwili utaagwa Saa 7 mchana kabla ya safari ya mazishi, kijiji kwao, Yombo, Bagamoyo, Pwani.
Abdul Maneno alijiunga na Yanga mwaka 1998 akitokea Sigara ya Dar es Salaam na akacheza hadi mwaka 2000 alipokwenda Msumbiji kumalizia soka yake.
Enzi zake Maneno alikuwa anafananishwa na mshambuliaji wa zamani wa Kimataifa wa Scotland, Denis Law aliyetamba Manchester United kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1973 alipokwenda kumalizia soka yake kwa majirani, Manchester City.
Marehemu ameacha mke, Zena Jaffar na watoto watatu ambao ni Abdul Jr (32), Jaffar (29), Mustafa (28). Mungu ampumzishe kwa amaani. Anin.
Abdul Maneno Kibavu, wa kwanza kulia katika kikosi cha Sigara mwaka 1996

TAZAMA MAHOJIANO ABDUL MANENO NA BIN ZUBEIRY NA ENZI ZA UHAI WAKE


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA