NAMUNGO FC YAZINDUKA NA KUICHAPA COASTAL UNION 2-0 CHAMAZI


TIMU ya Namungo FC imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuichapa Coastal Union mabao 2-0 jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Ritch Nkoli dakika ya 38 na Pius Buswita dakika ya 45’+2 huo ukiwa ushindi wa kwanza timu hiyo ikitoka kupoteza mechi tatu mfululizo kwa kufungwa 2-1 na Tabora United, 2-0 na Fountain Gate na 1-0 na Dodoma Jiji .
Kwa upande wao Coastal Union wanafikisha mechi tatu bila ushindi, kufuatia awali kutoa sare na KMC 1-1 , kabla ya kufungwa 1-0 na Mshujaa zote Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC Complex), Mwenge Jijini Dar es Salaam.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA