NGUSHI APIGA BAO PEKEE MASHUJAA YAICHAPA COASTAL UNION 1-0 MWENGE


BAO la dakika ya 14 la mshambuliaji Crispin Ngushi Mhagmaa limeipa Mashujaa FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC), Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Mashujaa FC wanafikisha pointi saba na kusogea nafasi ya pili, nyuma ya Singida Black Stars yenye pointi tisa baada ya wote kucheza mechi tatu, wakati Coastal Union inabaki na pointi moja kufuatia kucheza mechi mbili.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA