SERENGETI GIRLS YAWACHAPA MABINTI WA MOROCCO 5-3 UNAF


TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls leo imeendeleza ubabe katika michuano ya Kaskazini mwa Afrika (UNAF) baada ya kuichapa Morocco mabao 5-3 Uwanja wa Ariana Jiji la Pwani, Ariana Kaskazini Mashariki kwa Tunisia.
Mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Mwatima Mwarabu mawili, Yasinta Joseph Mitoga moja na Winfrida Gerlad mawili.
Huo unakuwa ushindi wa pili kwa Serengeti Girls kutoka ukanda wa CECAFA wakiwa kama waalikwa kwenye michuano hiyo baada ya kuichapa Misri 4-1 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Manispaa wa Kram mjini Kram.
Siku hiyo mabao ya Serengeti Girls yalifungwa na Mwatima Mwarabu mawili, Yasinta Joseph Mitoga na Jamila Rajab Mnunduka moja kila mmoja.
Katika michuano hiyo inayofikia tamati Septemba 9, Serengeti Girls watarudi Uwanja wa Ariana Jumamosi kuanzia Saa 10:30 jioni kadhalika kumenyana na wenyeji, Tunisia kukamilisha mechi zao.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA