SINGIDA BLACK STARS YAENDELEZA UBABE, YAICHAPA KMC 2-1 LITI


WENYEJI, Singida Black Stars wameendeleza wimbo la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuichapa KMC mabao 2-1 Uwanja wa CCM Liti mjini Singida.
Mabao ya Singida Black Stars inayofundishwa na Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems yamefungwa na Josephat Bada dakika ya 40 na Elvis Rupia dakika ya 57, wakati la KMC limefungwa na Redemtus Mussa dakika ya 49.
Huo unakuwa ushindi wa tatu kwa Singida Black Star baada ya awali kushinda mechi mbili ugenini dhidi ya Ken Gold 3-1 Jijini Mbeya na Kagera Sugar 1-0 mjini Bukoba.
Kwa KMC huo unakuwa mchezo wa pili kucheza bila ushindi, kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Union, nyumbani, Dar es Salaam wiki iliyopita. 


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA