SINGIDA YA KWANZA KUIFUNGA PAMBA, YAICHAPA 1-0 KIRUMBA


TIMU ya Singida Black Stars imeendeleza wimbi la ushindi katika mchezo wa nne mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Pamba Jiji FC bao 1-0 mchana wa leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Bao pekee la Singida Black Stars inayofundishwa na Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems limefungwa na kiungo Mghana, Emmanuel Kwame Keyekeh dakika ya kwanza tu ya mchezo huo.
Singida Black Stars inafikisha pointi na kuendelea kuongoza ligi, wakati Pamba Jiji FC iliyo chini ya Kocha Mserbia, Goran Kopunovic inabaki na pointi zake tatu baada ya timu zote kucheza mechi nne.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA