YANGA YAICHAPA CBE 1-0 PALE PALE ABEBE BIKILA BAO LA DUBE


KLABU ya Yanga imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, timu ya Benki ya Biashara Ethiopia, CBE SA (Commercial Bank of Ethiopia Sports Association) jioni ya leo katika mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 45’+1 na mchezo wa marudiano utafanyika Jumamosi ya Septemba 21 katika Uwanja ambao utathibitishwa na Yanga.
Mshindi wa jumla atakwenda Hatua ya 16 Bora inayochezwa kwa mtindo wa makundi.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA