ZAMALEK WAIPIGA AL AHLY KWA MATUTA NA KUTWAA SUPER CUP YA AFRIKA


TIMU ya Zamalek usiku wa jana imefanikiwa kutwaa taji la Super Cup ya Afrika baada ya ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 na mahasimu wao wa jadi, Al Ahly Uwanja wa Kingdom Arena Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Al Ahly walitangulia kwa bao la mshambuliaji Wessam Abou Ali dakika ya 44 kwa penalti kufuatia Akram Tawfik kuchezewa rafu na Hamza Mathlouthi, kabla ya Naser Mansy kuisawazishia Zamalek dakika ya 77, dakika moja tu tangu aingie kuchukua nafasi ya Seifeddine Jaziri akimalizia krosi ya Omar Gaber.
Katika mikwaju ya penalti, Yahia Attiyat Allah wa Al Ahly alikosa penalti muhimu na Wessam Abou Ali akagongesha mwamba na kuwapa Zamalek ambao penalti yao ya mwisho ilipigwa na Hossam Abdelmaguid.
Hilo linakuwa taji la tano la Super Cup ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa Zamalek. 






Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA