AZAM FC YAWAZIMA PRISONS PALE PALE MBEYA, YAWAPIGA 2-0 SOKOINE


TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo, winga Iddi Suleiman Nado dakika ya 12 na mshambuliaji mpya aliyesajiliwa kutoka Geita Gold iliyoshuka daraja, Nassor Saadun Hamoud dakika ya 43.
Kwa ushindi huo, Azam FC iliyo chini ya kocha Mmorocco Rachid Toussi inafikisha pointi 15 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya pili nyuma ya Singida Black Stars yenye pointi 16 za mechi sita. 
Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kupoteza mchezo wa leo ambao ni wa pili kufungwa, inabaki na pointi zake saba za mechi saba nafasi ya 12.

 



Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA